Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Dkt. Anna Mghwira ameyataka mashirika mengine yanayoshughulika na utunzaji wa mazingira kujifunza mbinu na maarifa bora ya kutunza mazingira kutoka shirika la Floresta Tanzania kwa juhudi za utunzaji wa mazingira hususani katika kupanda miti.

Akiongea na wananchi wa kijiji cha mungushi kata ya Masama Kusini wilayani Hai waliokusanyika katika shughuli ya uzinduzi wa programu ya siku thelasini ya upandaji wa miti Dkt. Mghwira amesma tuzo ya utunzaji bora kimkoa waliyoipata shirika la Floresta walistahili kuipata kutokana na juhudi na kujituma kwa shirika hilo katika kutunza mazingira

Aidha Mhe. Mkuu wa Mkoa amelitaka shirika hilo kuongeza juhudi zaidi kupanda miti katika maeneo ya barabara kuu inayounganisha mkoa wa Kilimanjaro na mikoa ya jirani. Akitolea mfano eneo la kuingilia na linalozunguka uwanja wa nde wa kimataifa wa Kilimanjaro KIA, Dkt. Mghwira amesma ni miongoni mwa maeneo yanayohitaji juhudi zaidi katika kupanda miti na kuitunza ili kulifanya eneo hilo liwe la kuvutia wageni wanapoingia mkoani Kilimamnjaro.

Dkt. Mghwira amekumbusha kuwa hadi kufikia mwezi disemba mwaka huu kazi ya kuotesha miti kuanzia wilaya ya Hai hadi Same iwe imeshakamilika ili nguvu na maarifa zaidi yaelekezwe kwenye kuitunza miti hiyo.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Floresta Tanzania Bwana Richard Mhina amemshukuru Dkt. Mghwira kwa kuunga mkono shughuli za shirika hilo kwa kuwapa ushirikiano wa mara kwa mara katika kuhakikisha kuwa kazi za shirika la Floresta zinatekelezwa katika mkoa wa Kilimanjaro.

One Reply to “FLORESTA NI MFANO WA KUIGWA – RC MGHWIRA”

  1. Kwa kweli kazi ya Upandaji Miti ni kazi njema sana na Itapendeza Zaidi mkiongeza Ufanisi wa Kufikia Tanzania nzima hasa kwa Maeneo ya Vijijini na ya pembezoni

Leave a Reply

Your email address will not be published.

You may use these <abbr title="HyperText Markup Language">HTML</abbr> tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

*

Hi, How Can We Help You?