SHIRIKA LA FLORESTA TANZANIA LINAWATANGAZIA WOTE NAFASI YA KAZI KAMA ILIVYOAINISHWA HAPO CHINI

Full time
Moshi
Posted 3 years ago

­­­­TANGAZO LA KAZI

SHIRIKA LA FLORESTA TANZANIA LINAWATANGAZIA WOTE NAFASI ZA KAZI KAMA ILIVYOAINISHWA HAPO CHINI

NAFASI:  14 za wawezeshaji

 

MAJUKUMU

Kutoa mafunzo Juu ya umuhimu wa afya ya ikolojia na uhifadhi wa mazingira katika ustawi wa maisha ya viumbe hai na uchumi wa kaya. Kuhakikisha wakulima waliopatiwa mafunzo tajwa hapo juu wanatumia mbinu bora za kilimo na tekinolojia mbalimbali zilizofundishwa. Kukusanya taarifa mbalimbali kutoka kwenye vikundi, watu binafsi na taasisi kadri zinavyohitajika. Kutoka taarifa ya maendeleo ya vikundi kila mwezi au mapema zaidi pale zinapojitajika kwa msimamizi wa kazi

 

SIFA ZA MWOMBAJI

 1. Awe na cheti cha Kilimo, Mazingira au cha kidato cha nne
 2. Awe anakubalika na jamii na mkazi wa eneo husika
 • Awe tayari kufanya kazi mahali popote atakapopangina na mwajiri
 1. Awe na ufahamu wa maswala ya kilimo na uhifadhi wa mazingira
 2. Awe na nguvu ya ushawishi
 3. Awe na umri kuanzia miaka 18
 • Awe mwepesi kuelewa na kuelewesha wengine
 • Awe mvumilivu na mwenyekujiheshimu
 1. Awe na uwezo wa kujisimamia mwenyewe katika kazi zake
  • SIFA MAALUMU (ADDED ATTRIBUTES)
 2. Wakulima wa mfano waliopo katika orodha ya Floresta watatewa kipaumbele katika kazi hii. Wanachama wa vikundi vya Floresta walio na sifa tajwa hapo juu watapewa kipaumbele

 

8.0 KAZI ZA MWEZESHAJI

Kama kiungo cha shirika na wanavikundi, utapaswa kufanya yafuatayo.

 1. Ni wajibu wa Muwezeshaji (wa ECC) kuhakikisha wanachama wanahudhuria katika mafunzo.
 1. Kutoa taarifa ya kazi kwa msimamizi wako (kwa kutumia form maalum) Taarifa hiyo/hizo zitawakilishwa kwa mwezi zikionyesha maendeleo ya kazi pamoja na changamoto ulizokutananazo ndani ya vikundi vyako kwa mwezi husika.
 • Kutoa ushauri kwa msimamizi wako juu ya utendaji wa vikundi
 1. Kuhudhuria mafunzo na mikutano ya kila mwezi ya wawezeshaji. Mkutano huu ni wa kuangalia matatizo uliyokutananayo kwenye vikundi, maendeleo ya kazi kwa kipindi cha mwezi mzima.Mkutano huu pia ni fursa ya msimamizi wako kutoa ushauri juu ya utendaji kazi.
 1. Kuongoza wanavikundi katika uanzishaji na usimamizi wa mashamba darasa, Pamoja na kufuatilia mwenendo mzima wa majaribio hayo.
 2. Kusimamia na kuhamasisha uanzishaji wa vitalu vya miti na upandaji miti
 3. Kutembelea vikundi kila wiki ili kuwajengea uwezo katika maswala ya kilimo, uhifadhi wa mazingira na utunzaji wa kumbukumbu
 4. Kutembelea wakulima wa kilimo hai, kuhamasisha uzalishaji wa bidhaa za kilimo hai pamoja na kusimamia Umoja wa Wazalishaji Kilimo Hai (UWAKIHA)
 5. Kuripoti changamoto zote anazokutanaa nazo katika kazi na namna alivyozifanyia kazi ili kutatua changamoto hizo
 6. Kusimamia mradi wa mbuzi kama miongozo inavyoelekeza

 

Zingatia:

 1. YEYOTE MWENYE SIFA ZILIZOAINISHWA HAPO JUU ALETE MAOMBI YAKE OFISI YA FLORESTA KWA ANUANI IFUATAYO. Mkuu wa Idara (Environmental Restoration), Floresta Tanzania, S.L.P 7764 Moshi au kwa barua pepe jobs@floresta.co.tz. MWISHO WA KUWASILISHA MAOMBI HAYO NI TAREHE 30/4/2019
 2. Mwombaji katika barua yake aandike eneo analotoka pamoja na namba ya simu.Karibuni tushirikiane KUIPONYA ARDHI NA WATU WAKE
 • Tangazo hili limetolewa na Mkurugenzi wa shirika la Floresta Tanzania ndugu Richard Mhina.

Job Features

Job CategoryMafunzo ya Afya

Apply Online